Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba ya Mbappe itakuwa hapa

Nyumba Ya Mbappe Spain Nyumba ya Mbappe itakuwa hapa

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kumekuwa na taarifa, mama wa nyota wa kimataia wa Ufaransa na klabu ya Paris Saint German, Kylian Mbappe, Fayza Lamari yuko Hispania kutafuta nyumba kwa ajili ya mwanaye atakapojiunga na miamba ya la Liga, Real Madrid.

Sasa, kilichopo ni nyumba hiyo inapatikana maeneo ya La Moraleja na ni umbali wa dakika 10 kufika Valdebebas, mahala ulipo uwanja wa mazoezi wa miamba hiyo na ndipo yalipo makao makuu ya klabu hiyo.

Eneo la pili ambalo mama Mbappe anafikiri angepata nyumba huko ni Finca na mastaa wengi wa Madrid ndiko wanakoishi kwa sasa.

Mama wa nyota huyo anataka nyumba iliyo karibu na uwanja ambao Madrid inafanyia mazoezi ili iwe rahisi kwenye harakati za kila siku za mwanaye kuwahi mazoezini na kurudi nyumbani.

Mbappe mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake na PSG unamalizika mwisho wa msimu huu na inaaminika atajiunga na Madrid kwa usajili huru.

Licha ya kwamba atajiunga kama mchezaji huru bado Madrid itatakiwa kulipa pesa nyingi kuliko zile ambazo ililipa kwa Jude Bellingham.

Kwa mjumuisho wa mshahara na bonasi ya usajili Mbappe huenda akaigharimu Madrid zaidi ya Pauni 114 milioni ndani ya kipindi kifupi tu.

Mbali ya pesa dili la Mbappe linahusisha pia usajili wa mdogo wake Ethan Mbappe ambaye anatakiwa asajiliwe Madrid kama sehemu ya dili na pia pesa itatakiwa itoke ili kukamilisha uhamisho wake.

Mbappe kwa sasa mama yake ndio wakala wake na amekuwa akihusika kwenye mazungumzo na masuala mengine ya nje ya uwanja juu ya staa huyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari kutoka Hispania Relevo ameeleza Fyza amekuwa nchini Hispania mara kadhaa ikiwa pamoja na kufanya mazungumzo ya dili, pia kufanya maandalizi kabla ya mwanawe hajatua.

Chanzo: Mwanaspoti