Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyuma Mwiko wanasubiri tiketi za Sandakalawe - Ahmed Ally

Yanga Mashabiki R.jpeg Nyuma Mwiko wanasubiri tiketi za Sandakalawe - Ahmed Ally

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewapiga dongo wapinzani wao Yanga SC kwa kugawa tiketi bure kwa mashabiki zao kuelekea mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Ahmed amesema kuwa, mchezo wa Simba na Al Ahly ndio mchezo mkubwa katika michezo yote minne ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Mechi yetu sisi Simba na Al Ahly ndio kubwa zaidi kuliko mechi ya Nyuma Mwiko, sisi mpaka sasa tuna mikoa 10 ilishaandaa mabus kuja kuangalia mechi yetu kwa Mkapa na tiketi wamejinunulia wenyewe sio za bure au za kugawiwa.

"Kwa hiyo sisi mechi yetu Mashabiki wanajinunulia tiketi za mechi na sio kama Nyuma Mwiko ambao wanasubiri tiketi za Sandakalawe, sisi Simba ni kubwa zaidi Afrika Mashariki hatuwezi kuweka tiketi za bure," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live