Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota watatu waachwa Dar, Yanga ikiifata Medeama

Ngushi Tresss.jpeg Crispin Ngushi

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha wachezaji 24 wa Yanga kimeondoka alfajiri ya leo kuwafuata Medeama SC, huku kocha mkuu Miguel Gamondi akiweka wazi kuwa dakika 180 za mechi mbili za kwaza zimempa mwanga sasa akili yote kwenye mchezo wa Ijumaa.

Wachezaji watatu wa timu hiyo wameachwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo majeraha ambao ni, Crispin Ngushi, Denis Nkane na Joyce Lomalisa.

Nyota walioenda ni Dickson Job, Nickson Kibabage, Kouassi Yao, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, PacĂ´me Zou-zoua, Jonas Mkude, Zawadi Mauya, Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli. Wengine ni Farid Mussa, Mahlatsi Makudubela, Moloko, Musonda, Mzize, Konkoni, Diarra, Metacha , Mshery, Bacca na Bakari Mwamnyeto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: