Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wanne watemwa Simba, Morrison awahishwa hospitali

Bm33 Pic Data Nyota wanne watemwa Simba, Morrison awahishwa hospitali

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author KIKOSI cha Simba kimeondoka nchini asubuhi ya leo Ijumaa Desemba 18 na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuelekea jijini Harare, Zimbabwe na watakaa kambi hapo kwa siku tano kabla ya kucheza na FC Platinum.

Simba watacheza mechi ya mzunguko wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa Desemba 23 mwaka huu.

Simba chini ya kocha mkuu Sven Vandenbroeck wameondoka na wachezaji 24, akiwemo nyota mpya aliyesajiliwa dirisha dogo Mganda Taddeo Lwanga huku wengine wanne wakibaki nchini kwa sababu mbalimbali ikiwemo Bernard Morrison.

Meneja wa Simba, Abass Selemani amesema wachezaji waliobaki ni Morrison ambaye anaumwa na alishindwa kufanya mazoezi na wenzake na leo Ijumaa atapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz