Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa zamani wa Lepzig afariki Dunia

Agyemang Diawusie Germany Agyemang Diawusie (25)

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa RB Leipzig ya Ujerumani Agyemang Diawusie (25), amefariki dunia.

Winga huyo aliyewahi kuichezea Ujerumani katika kikosi cha vijana walio chini ya umri wa miaka 19 amefariki ghafla na sababu za kifo chake bado hazijatajwa.

Katika msimu huu Diawusie alikuwa akiichezea klabu ya Jahn Regenburg ya Ujerumani iliyopo katika daraja la tatu.

Klabu hiyo imetoa taarifa za msiba huo kwa ujumbe uliosomeka ”Jumanne hii, klabu yetu imepata habari za kusikitisha kuwa mchezaji wetu Agyemang Diawusie amefariki. Klabu imeshikwa na mshtuko na majonzi mazito”.

Nao wadau mbalimbali wa soka kutokea nchini Ujerumani wanaendelea kutuma salamu zao za pole kwa familia, ndugu, jamaa na mashabiki wote wa soka walioguswa na msiba huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live