Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa zamani England afariki Dunia

Bowles Nyota wa zamani wa QPR, Manchester City na Timu ya Taifa England, Stan Bowles

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa QPR, Manchester City na Timu ya Taifa England, Stan Bowles amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa ‘Alzheimer’

Bowles ambaye alikuwa mmoja wa vipaji bora nchini England wakati wake kama mchezaji aligundulika na ugonjwa wa neva mnamo 2015.

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya klabu hiyo QPR imesema: “Ni kwa moyo mzito tumegundua kwamba nyota wa QPR Stan Bowles amefariki dunia jioni ya leo (Jumamosi), akiwa na umri wa miaka 75.”

NB: ‘Alzheimer’s’ ni aina ya ugonjwa wa mfumo wa neva ambao kwa kawaida huanza taratibu na hatimaye huathiri kumbukumbu, fikra na tabia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live