Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa Simba, Yanga wakutana Muhimbili, wapima afya!

SIMBA YANGA VIPIMO Nyota wa Simba, Yanga wakutana Muhimbili, wapima afya!

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Simba SC na wa Yanga SC, jana wamefanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi, 2022-23.

Wachezaji hao walionekana kupima vipimo mbalimbali vya afya ikiwemo moyo ambapo baada ya vipimo, nyota hao walipata nafasi ya kupiga stori mbili tatu kisha kila mmoja kuelekea kwenye majukumu yake.

Kwa mujibu wa daktari wa Simba SC, Edwin Kagabo, wachezaji wamepimwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo ili kuhakikisha wanaanza msimu wakiwa fiti.

Timu nyingi duniani zimeweka utaratibu wa kuwafanyia vipimo wachezaji kabla ya kuanza msimu mpya ili kuhakikisha usalama wao baada ya kutoka mapumzikoni.

“Huu ni utaratibu ambao upo duniani kote. Leo wachezaji wetu wamefanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya msimu mpya,” alisema Kagabo.

Simba wanaondoka leo mchana wakiwa na nyota wao wapya waliowasajili pamoja na wale waliokuwa nao msimu uliopita huku baadhi ya wazama wakisalia jijini Dar kutokana na majukumu ya timu ya taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live