Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa Bayern ajeruhiwa fuvu la Kichwa

Jude X Alpho.jpeg Nyota Bayern ajeruhiwa fuvu la kichwa

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa klabu ya Bayern Munich, Alphonso Davies amegundulika kuchubuka fuvu la kichwa baada ya kuumia jana katika mchezo dhidi ya klabu ya Borussia Dortmund.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya magoli 2-2 baada ya Bayern kuongoza na kusawazishiwa na Borussia ambapo beki Alphonso Davies alikutana na hatarri na kushindwa kuendelea na mchezo huo.

Alphonso Davies alikanyagwa kichwani na mchezaji wa klabu ya Borussia Dortmund Jude Bellingham wakati wanagombea mpira na kumfanya mchezaji huyo kupata majeraha.

Baada ya mchezo huo mchezaji Jude Bellingham alituma salamu za pole kwa mchezaji huyo ambaye alimsababishia majeraha huku kocha wa klabu ya Bayern Munich Julien Nagelsman akionesha kutokufurahishwa na tukio hilo na zaidi refa wa mchezo huo kutokutoa adhabu yoyote.

Baada ya mchezo huo kocha huyo aliweza kuzungumza

“Amempiga usoni. Sheria ziko wazi. Kuna tuhuma za mtikisiko. Hilo ni la kushangaza kwa teke la uso” kocha huyo ameonesha kutokufurahishwa na kilichotokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live