Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa Arsenal afariki Dunia

Whatsapp Image 2024 06 15 At 3 54 48 Pm Nyota wa zamani wa Arsenal na Everton Kevin Campbell amefariki dunia

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Arsenal na Everton Kevin Campbell amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 54.

Mshambuliaji huyo aliugua muda mfupi na hivi majuzi alilazwa Hospitalini kutokana na ugonjwa unaoathiri Kinga ya Mwili unaojulikana kama Sepsis uliopelekea kifo chake.

Gwiji huyo wa Uingereza aliingia katika kikosi cha kwanza cha Arsenal mwaka 1988, kabla ya kucheza mechi 213 akiwa na The Gunners.

Alijiunga na Klabu ya Everton na kuichezea kati ya 1999 na 2005, ambapo anakumbukwa kwa mabao yake tisa katika mechi tano ambayo aliiokoa klabu hiyo kushuka daraja muda mfupi baada ya kujiunga kwa mkopo.

Campbell mafanikio yake ni pamoja na kushinda Ligi Daraja la Kwanza, Kombe la FA, Kombe la Ligi na Kombe la Washindi wa Kombe la Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live