Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota sita wa Simba kuikosa Biashara United

Watakokosa Mechi Miongoni mwa Nyota wa Simba watakaoikosa mechi ya Kagera

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi ikiwa Leo ndio wanatupa karata yao ya kwanza katika Msimu wa Ligi kuu Bara 2021/2022.

Kuelekea mchezo huo nyota sita wa Simba wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Karume, Mara kutokana na sababu mbali mbali.

Nyota hao ni Ibrahim Ajibu ambaye ni kiungo mshambuliaji, huyu ana matatizo ya kifamilia pamoja na Sadio Kanoute ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Mwingine ni beki wa kati, Joash Onyango ambaye aliumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kugongana na mchezaji mwenzake kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Kiungo mwandamizi, Jonas Mkude, huyu anatajwa kutokuwa sehemu ya kikosi na nyota mwingine ambaye ataukosa mchezo wa leo ni Bernard Morisson ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu hii ni mechi yake ya pili.

Vile vile Taddeo Lwanga ambaye ni kiungo atakosekana kwenye mchezo wa leo kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu ambayo alionyeshwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga baada ya kuonyeshwa kadi za njano mara mbili.

Kuhusu mchezo wa leo, Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema kuwa wanahitaji kupata matokeo mazuri hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita wa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga.

Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbu kumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Hisani Jumamosi iliyopita dhidi ya wapinzani wao wa Jadi Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live