Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Taifa Stars afariki Dunia

Karume Songoro Mz Nyota Taifa Stars afariki Dunia

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Yanga Sports Club, Kagera Sugar, Pamba ya Mwanza, Moro United, Kahama United, 82 Rangers, Karume Jumanne Songoro (43) amefariki Dunia jana asubuhi Aprili 15, 2024 mjini Kahama alipokuwa akiishi na familia yake.

Karume alikuwa anasumbuliwa na Saratani na misuli ambayo alikuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.

Karume Songoro aliyezaliwa Machi 24, 1982 aliibukia Buluba ya Shinyanga, kabla ya kuhamia Lumumba Rovers na baadaye Toto African zote za Mwanza mwaka 1998.

Mwaka 1999 alisajiliwa Yanga SC ambako baada ya miezi kadhaa akaachwa na kutimkia 82 Rangers ya Shinyanga ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa Kahama United kufuatia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kujivua umiliki.

Mwaka 2004 akaenda Moro United hadi mwaka 2005 akahamia Kagera Sugar, kabla ya kwenda Rwanda kuchezea Rayon Sport.

Mara ya mwisho Karume Songoro ambaye amewahi pia kuchezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars - alichezea timu ya Geita Gold Mine nam mwaka 2014-215.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live