Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Stars waliokwea pipa hawa hapa

15980 Samatta+pic Nyota Stars waliokwea pipa hawa hapa

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen raia wa Denmark, ametangaza kikosi kinachokwenda kuiwakilisha nchi katika michuano ya kufuzu Afcon, huko nchini Equatorial Guinea, mechi yao ya kwanza itapigwa Machi 25 na wenyeji.

Kabla ya kuivaa  Equatoria Guinea, Poulsen alikipima ubavu kikosi chake na mechi za kirafiki mbili dhidi ya Harambee Stars ya  nchini Kenya, ambapo mechi ya kwanza ilichapwa mabao 2-1.

Leo Jumanne ya machi 23, 2021 Poulsen ameweka wazi majina ya wachezaji watakaosafiri kwenda  nchini Equatoria Guinea kucheza michuano hiyo.

Kikosi hicho kinaundwa na  Aishi Manula, Metacha Mnata, Juma Kaseja(makipa ), Shomary Kapombe, Isreal Mwenda,Erasto Nyoni, Bakari Mwamnyeto, Kelvin Yondani,Kennedy Juma, Laurent Alfred, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Nickson Kibabage, Yassin Mustapha, Simon Msuva, Hassan Dilunga.

Wengine ni Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, Feisal Salum 'Fei Toto', Himid Mao, Salum Abubakar 'Sure Boy', Farid Mussa,Iddy Suleiman Nado, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco, Yohana Mkomola, Shaban Chilunda,Deus Kaseke, Abdul Suleiman na Ayub Lyanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz