Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Simba aangua kilio uwanjani

Sefrgtg Nyota Simba aangua kilio uwanjani

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nahodha wa timu ya vijana ya Simba chini ya miaka 17, Abdul Salum 'Camavinga' ameangua kilio baada ya timu yake kupoteza mchezo wa kwanza katika ligi hiyo dhidi ya Yanga kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Camavinga ambaye alionyesha kiwango bora katika mchezo huo, ilibidi abembelezwe na wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi la Simba kutokana na kipigo hicho ambacho kimewashusha kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo ya vijana.

Kocha wa Simba, John Bocco ambaye alisimama kwa dakika 70 za mchezo huo, aliwatia moyo wachezaji wake ambao nyuso zao zilionekana kuwa na simanzi huku upande wa pili ikiwa kicheko.

Akiwa na maumivu ya kupoteza mchezo huo wa kwanza kwa Simba katika ligi ya vijana, Camavinga alikimbilia katika vyumba vya kubadilishia nguo na kufuatiwa na wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi huku wakiwaacha Yanga wakitamba.

Matokeo hayo yameifanya Simba yenye pointi 17 kushushwa na Azam (20) ambayo katika mchezo wa mapema iliifunga JKT Tanzania kwa bao 1-0 kwenye uwanja huo. Awali, Simba na Azam wote zilikuwa na pointi sawa 17, zilitofautishwa na mabao.

Simba inayonolewa na Bocco ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika mchezo huo kupitia kwa Athuman Idd katika kipindi cha pili lakini Yanga ilitoka nyuma na kufunga mara mbili.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Chitunzi Masaka na Hamis Idd ambaye aliingia kipindi cha pili, kwa zaidi ya dakika 10 vijana wa Bocco waliweka kambi katika nusu ya wapinzani wao.

Hata hivyo, Yanga ilikuwa imara na kwa kuwa ilikuwa mbele huku wachezaji wake walionekana kupoteza muda jambo ambalo lilionekana kumkwaza Bocco aliyekuwa akitazama saa kila wakati.

Licha ya matokeo hayo, Simba bado ina nafasi ya kupigania ubingwa katika ligi hiyo kutokana na kusaliwa kwa michezo mitano mbele yao. Kabla ya mchezo wa leo, Yanga ilikuwa nafasi ya saba ikiwa na pointi 10 hivyo kwa sasa imefikisha pointi 13.

Chanzo: Mwanaspoti