Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Real Madrid aoneshwa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza

Toni Kroos Red Card Toni Kroos akioneshwa kadi nyekundu

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Real Madrid Toni Kroos amepata adhabu ya kadi nyekundu kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka ambapo kadi hiyo ameipata kwenye mchezo wa hapo juzi walipolazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Girona.

Kroos amecheza Ligi Kuu ya Ujerumani na Hispania akiwa na Bayern Liverkusen, Bayern Munich kabla ya kutjiunga na real Madrid mwaka 2014.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ujerumani alipata kadi nyekundu juzi jumapili baada ya kumchezea vibaya Aleix Garcia huku Girona wakionekana kuwalazimisha sare Madrid wakiwa Santiago Bernabeu.

Kutokana na hiyo kadi ilimfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kulazimika kuondoka uwanjani katika dakika ya 90+ 1 na mchezo huo kumalizika kwa sare.

Baada ya kucheza Bundesliga kwa mara ya kwanza mwaka 2007 na kukua taratibu hadi kuwa mchezaji nyota wa Bayern, Kroos alisajiliwa na Madrid Julai 2014, siku chache baada ya kuisaidia timu yake ya Taifa kushinda Kombe la DuniA 2014.

Ameshinda Ligi ya Mabingwa mara tano, ametwaa mataji matatu ya Bundesliga na mataji matatu ya LaLiga, na kuongeza ushindi mara tano wa Kombe la Dunia la Klabu. Amefunga mabao 59 na kuongeza pasi za mabao 130.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live