Sat, 15 Oct 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mchezaji wa Manchester United Mason Greenwood ameripotiwa kutiwa mbaroni tena kwa kinachoelezwa kuwa ni amevunja masharti ya dhamana.
Mamlaka ya polisi Jijini Manchester imeripoti leo Jumamosi, Oktoba 15.
Greenwood alikamatwa na kisha kuachiwa kwa dhamana mwanzoni mwa mwaka huu kwa tuhuma za kumbaka na kumshambulia msichana mmoja ambaye aliibuka na madai hayo mtandaoni.
Klabu ya Manchester United ilitangaza kumsimamisha, Kampuni ya NIKE pamoja na makampuni mengine ambayo yalikuwa yakishirikiana naye Kibiashara yalijiondoa baada ya tuhuma hizo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live