Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Mamelodi walioko Timu ya Taifa wapewa ndege maalum kuja Tanzania

Mamelodi Ms Nyota Mamelodi walioko Timu ya Taifa wapewa ndege maalum kuja Tanzania

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Mamelodi Sundowns waliopo katika Kikosi cha Taifa cha Afrika Kusini 'Bafana Bafana' watasafiri kwa ndege kutoka Algeria moja kwa moja hadi Tanzania, wakati huo huo wachezaji wa Chiefs na Maharamia Orlando Pirates watarudi nyumbani Afrika Kusini.

Afrika Kusini ambao wapo nchini Algeria kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya FIFA Series 2024, walicheza mchezo wa kwanza na Andorra, Machi 21, 2024 na kutoa sare ya bao 1-1 kabla ya mchezo wa jana Machi 26, na wenyeji Algeria na kutoa sare ya bao 3-3.

Mamelodi watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Wananchi Yanga SC katika mchezo wa robo fainali ya CAFCL utakaopigwa Jumamosi ijayo, Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live