Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Liverpool nje miezi minne

Melo Arthur.jpeg Arthur Melo

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Liverpool, Arthur Melo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne baada ya kuumia katika mazoezi ya timu hiyo akimpa presha Jurgen Klopp kwani alimsajili kwa mkopo dirisha la usajili la kiangazi mwaka huu.

Kiungo huyo wa kimataifa Brazil amecheza mechi moja tu tangu alipotua kwa mkopo akitokea Juventus lakini sasa atasubiri nje hadi atakapopata nafuu baada ya kuumia mazoezini.

Kocha wa Liverpool, Klopp amethibitisha kuumia kwa kiungo huyo kabla ya mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal ambao ulichezwa jana hadi tunaingia mtamboni.

"Kweli Melo amepata jeraha, ndiye mchezaji pekee aliyeumia kikosini, Aliumia mazoezini kabla ya mechi yetu ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Rangers (wiki iliopita), ni kawaida kwa mchezaji kupata maumivu ya misuli, tunasubirimajibu ya daktari watasema nini, vilevile tutapewa maelezo muda ambao atakaa nje," alisema Klopp wiki iliopita.

Sasa kwa mujibu wa taarifa Melo atafanyiwa upasuaji na atarudi dimbani mwakani, kiungo huyo kutoka Brazil atakosa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nmwezi ujao, Qatar.

Liverpool ilimsajili Melo kwa mkopo wa msimu mzima na kutoa Pauni 4 milioni, mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya aliyocheza ilikuwa dhidi ya Napoli, majogoo wa Anfield wakipokea kichapo cha mabao 4-1. Katika mechi hiyo kiungo huyo alicheza dakika 13 tu baada ya kuingia akitokea benchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live