Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Ihefu kuoga minoti

Ihefu Yapanda Ligi Kuu @binzubeiry Nyota Ihefu kuoga minoti

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

WASHINDWE wenyewe tu! Wachezaji wa Ihefu SC wamejazwa upepo baada ya mabosi wao kuwatangazia dau kubwa kwa kila mechi watakayoshinda kuanzia sasa ili kuinusuru timu hiyo isishuke daraja, baada ya hali yao ndani ya Ligi Kuu Bara kuwa mbaya.

Ihefu iliyopanda msimu huu kupitia Play Off, wako nafasi tatu za chini na kuamsha presha kwa mashabiki katika ishu ya kushuka daraja ikiwa imebaki mechi 10 tu kuamua hatma yake, lakini mabosi nao waliitana chemba na kupanga mikakati kuhakikisha jahazi halizami mikononi mwao.

Katibu Mkuu wa Ihefu, Athuman Mndolwa alisema katika kuhakikisha timu hiyo inabaki Ligi Kuu, uongozi umeongeza bonasi kwa wachezaji ikiwa ni njia kuamsha upya morali kwa nyota wao, ambapo kila mechi imetengewa fungu lake.

Licha ya kutotaja kiwango kilichoongezwa akidai ni siri ya ndani, Mndolwa alisema dau walilotenga kwa kila mechi ni nono ambalo kwa mchezaji wa Ligi Kuu ni kiwango bora ambacho kitachochea kujituma zaidi.

“Ishu ya kiwango kilichoongezwa ni siri yetu uongozi na wachezaji, lakini tulikaa nao tukakubaliana kuongeza kutoka ile ya awali, lengo kubwa ni kushinda kila mechi na kuibakiza timu Ligi Kuu,” alisema Mndolwa.

Kigogo huyo aliongeza kutokana na malengo yao, waliamua kutoa likizo ya wiki moja ambapo kwa sasa tayari timu imeshaingia kambini ikiendelea kujifua kujiandaa na mwendelezo wa mashindano yao.

“Kwa sasa hakuna kingine kinaangaliwa tofauti na timu katika kukwepa kushuka daraja, tunashukuru tuna umoja na mshikamano na tumedhamiria kutofanya makosa kwenye hizi mechi 10,” alisema

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz