Nyota wa zamani wa England Alfie Mawson (29), amelazimika kustaafu kutoka kwenye soka kutoka na majeraha kadhaa ya goti.
Mawson ambaye alikuwa akichezea Wycombe tangu kuanza kwa msimu huu alijiunga na Fulham mwaka 2018 akitokea Swansea City.
Akizungumza katika tovuti ya Wycombe, Mawson amesema ” hii inaweza ikawastua baadhi ya watu lakini kwangu ni kitu ambacho kimekuwa kinakuja kwa muda mrefu tu. Baada ya kuongea na wataalamu, familia yangu na klabu, nimefikia uamuzi mgumu wa kustaafu”
”Nitaendelea kuwa shabiki wa Wycombe, sitaki kuaga na kuondoka maana nina deni kubwa, klabu hii imenifanyia mengi sana, nitawakumbuka sana”.