Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Dodoma asajiliwa nchini Iraq

Opareeeeeeee Nyota Dodoma asajiliwa nchini Iraq

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Collins Opare amejiunga na timu ya Al Zawraa SC, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Iraq kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Opare tayari yupo mjini Baghdad, yalipo maskani ya timu hiyo na juzi alicheza mechi yake ya kwanza ndani ya Al Zawraa dhidi ya Mosul, ambayo ilimalizika kwa suluhu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Opare aliyefunga mabao tisa kwa msimu ulipita akiwa na Dodoma, alisema msimu huu alikuwa na ofa mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo kutoka Simba lakini amechagua kujiunga na Al Zawraa.

"Simba na timu nyingine za Tanzania zilionyesha nia ya kutaka nisaini kwao lakini kuna vitu havikukamilika ndio maana nimekuja huku (Iraq).

Kwa sasa sina maneno mengi, nadhani uongozi wangu umefanya kila kitu ndio maana nipo hapa na naamini nitafanya vizuri katika majukumu haya mapya," alisema Opare.

Opare alitua nchini msimu wa 2021/22 akisajiliwa na Biashara United iliyokuwa Ligi Kuu kwa msimu huo, lakini baadaye timu hiyo ilishuka daraja na Opare kusajiliwa na Dodoma Jiji kabla ya sasa kutua Al Zawraa.

Chanzo: Mwanaspoti