Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota City ajichomoa Ligi Kuu

Mbeya Cittttty Nyota City ajichomoa Ligi Kuu

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Mbeya City, Maulid Shaban amesema kutokana na vita ya kupanda Ligi Kuu kuonekana ngumu, kwa sasa anaelekeza nguvu kwenye kuwania ufungaji bora, huku akiwashtua mabeki wa timu hiyo.

Mbeya City ilishuka daraja msimu uliopita na hadi sasa imekusanya pointi 38 ikiwa nafasi ya saba na zimebaki mechi sita kuamua hatma yao ya kurejea au kusubiri msimu mwingine.

Shaban alisema kwa sasa ni wazi mbio za kupanda zinaonekana kuwa ngumu kutokana na pointi walizoachwa na vinara Ken Gold wenye alama 53 (kabla ya mechi ya juzi) hivyo lazima aangalie njia nyingine ya kutokea.

Alisema licha ya kiwango bora alichonacho, lakini hafurahishwi na matokeo ya jumla ya timu hiyo, akieleza licha ya mastraika kufanya kazi yao vyema, ila tatizo lipo kwa beki kuruhusu mabao.

“Mimi ni mchezaji, kuna maisha baada ya Mbeya City, lazima niangalie namna ya kupambania ufungaji bora kuweza kujitangaza zaidi, tatizo lipo kwa beki wanaoruhusu mabao.”

“Japokuwa lolote linaweza kutokea, ila kiuhalisia hesabu ni kama zinagoma, tunapaswa kupambana kwa sasa kila mechi kwetu kuwa fainali ili kuona tunahitimishaje msimu,” alisema nyota huyo mwenye mabao 13.

Hadi sasa nyota wa Ken Gold, William Edgar ndiye kinara wa mabao akiwa na 16, akifuatiwa na staa wa Biashara United, Boban Zirintusa huku Frank Gamba (TMA) akiwa nayo 11 sawa na Oscar Mwajanga wa Mbeya Kwanza.

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Mathias Wandiba alisema baada ya sare mbili mfululizo dhidi ya Stand United na Biashara United, wanaenda kusahihisha makosa eneo la beki ili mchezo ujao na Pamba Jiji ugenini wafanye kweli.

Chanzo: Mwanaspoti