Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota Al-Ahly amfunika Chama mchezaji Bora wa wiki CAF

Mahmoud Kahraba Nyota wa Al Ahly, Mahmoud Kahraba

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Al Ahly, Mahmoud Kahraba ameshinda mchezaji bora wa wiki mzunguko wa tano Ligi ya Mabingwa Afrika akimzidi Clatous Chama wa Simba ambaye walikuwa wakichuana kwa ukaribu katika saa 24 za kupiga kura kwenye ukurasa wa Twitter wa CAF rasmi unaohusika na mashindano ya ngazi ya klabu.

Kahraba amepata asilimia 49.3 na Chama asilimia 43.5 katika kura zote zilizopigwa 255,521 huku Percy Tau akipata asilimia 4.9 na wa mwisho Sadio Kanoute wa Simba asilimia 2.2

Ktika mechi za mzunguko wa Tano, Chama alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya goli dhidi ya Horoya katika ushindi wa bao 7-0 waliopata Simba.

Mahmoud Kahraba alifunga mabao matatu dhidi ya Cotton Sports katika ushini wa bao 4-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live