Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota 25 kukipiga na Zanzibar Heroes

Mastaa Stars KK Nyota 25 kukipiga na Zanzibar Heroes

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars', Adel Amrouche ametaja kikosi cha wachezaji 25 watakaoingia kambini kesho kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes'.

Mchezo huo utakaopigwa Desemba 27 ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar uliofanyiwa marekebisho makubwa.

Kikosi hicho kinaundwa na makipa Kwesi Kawawa (Karlslunds IF), Beno Kakolanya (Singida Fountain Gate) na Aishi Manula wa Simba huku mabeki wakiwa ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Nickson Kibabage (Yanga), Israel Mwenda, Mohamed Hussein 'Tshabalala' wa Simba.

Wengine ni Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Adam Kasa (IFK Haninge), Zion Chebe Nditi (Aldershot Town), Mark John (Kingston FC) na Miano Danilo wa Villena CF.

Viungo ni Adolf Bitegeko (Volsungur IF), Yusuph Kagoma (Singida FG), Roberto Yohana (Fofar Athletic), Mzamiru Yassin (Simba), Edwin Balua (Tanzania Prisons), Said Hamis (Jedinstov Ub), Tarryn Allarakhia (Wealdstone) na Sospeter Bajana wa Azam.

Washambuliaji wanaongozwa na Simon Msuva aliyeachana na klabu ya JS Kabylie ya Algeria baada ya kuvunjiwa mkataba mapema Desemba hii, Ladaki Chasambi (Mtibwa Sugar), Kibu Denis (Simba) na Abdul Suleiman 'Sopu' anayekipiga kunako Azam FC.

Chanzo: Mwanaspoti