Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota 25 Timu ya Taifa ya Ufaransa kuelekea EURO 2024

Dasc Ufaransa Nyota 25 Timu ya Taifa ya Ufaransa kuelekea EURO 2024

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya michuano ya Euro 2024.

Kiungo wa zamani wa Chelsea, N’Golo Kanté amejumuishwa kikosini sambamba na nyota kadhaa wakiwemo beki wa Arsenal, William Saliba, kiungo wa PSG, Warren Zaire-Emery, mshambuliaji Olivier Giroud na Kylian Mbappé.

Winga wa Crystal Palace, Michael Olise, nyota wa Chelsea, Malo Gusto, Axel Disasi na Christopher Nkunku hawajaitwa.

Nyota wengine ambao hawajajumuishwa ni pamoja na Mohamed Simakan, Jean Clair Todibo, Ben Yedder, Mattéo Guendouzi, , Jean-Philippe Mateta, Jordan Veretout na Moussa Diaby.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live