By OLIPA ASSA NA THOMAS NG'ITUYANGA imeendelea na mazoezi ikiwa ni siku ya pili tangu itangaze kuanza kambi huku wachezaji 15, wapya watatu na 12 wa zamani walikuwa wakijifua katika Uwanja wa Chuo cha Sheria Simu 2000, kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mazoezi hayo yanafanywa chini ya kocha wa Yanga B, Said Maulidi 'SMG' na miongoni mwa nyota waliokuwa nao tangu msimu ulioisha ni kipa Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili, mabeki Adeyum Saleh, Paul Godfrey na Said Makapu.
Wakati viungo ni Feisal Salum 'Fei Toto', Abdulaziz Makame na Deus Kaseke, washambuliaji ni Adam Kiondo wa timu B, Juma Mahadhi na Ditram Nchimbi.
Wapya ambao Yanga imewasajili na wameungana na wenzao katika mazoezi hayo ni beki Yassin Mustapha (Polisi Tanzania), straika Wazir Junior (Mbao FC) na kiungo Zawadi Mauya (Kagera Sugar).
MAZOEZI YALIVYOKUWA
Kaseke bado anaonekana yupo fiti katika mazoezi hayo, alikuwa mwepesi wakupiga mipira, kasi na pumzi.