Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota 10 Kombe la Dunia tishio kwenye usajili

Sofiane Amrabqt.jpeg Sofyan Amrabat

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michuano ya kombe la dunia huko Qatar inaelekea ukingoni kwa michezo miwili pekee kusalia, Jumamosi ya Disemba 17 tukitegemea kushuhudia mchezo wa kuwania mshindi wa tatu katika ya Croatia na Morocco pamoja na ule wa Fainali siku ya Jumapili ya Disemba 18 baina ya Argentina na bingwa mtetezi Ufaransa.

Wachezaji nyota takribani 10 wameingia katika rada za vilabu kadhaa barani Ulaya kuelekea dirisha dogo la usajili majira ya baridi. Baadhi ya Wachezaji hao nyota ni pamoja na beki Kisiki wa Croatia pamoja na klabu ya RB Leipzig, Josko Gvardiol (20) anayewaniwa na vilabu vya Chelsea pamoja na Real Madrid.

Mshambuliaji wa klabu ya PSV Eindhoven na taifa la Uholanzi, Cody Gapko (23) amekuwa katika kiwango bora akiwa na taifa lake katika michuano ya Kombe la Dunia kiasi cha kuwavutia miamba Manchester United na kuwekwa katika orodha ya juu kama kipaumbele cha kwanza katika usajili ili kuziba pengo la Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo.

Aidha viungo wa Taifa la Morocco Sofyan Amrabat (Fiorentina ya Italia) pamoja na Azzadinne Ounahi (Angers ya Ufaransa) nao wameingia katika rada za vilabu kutoka Ligi Kuu England (EPL) kutokana na mchango wao mkubwa kwenye Kombe la Dunia wakiwa na Morocco. Amrabat anawindwa na klabu ya Liverpool huku Azzadinne Ounahi akiwindwa na vilabu vitatu kutoka EPL, Westham United, Leicester city pamoja na Wolves.

Wachezaji wengine waliong'aa katika katika kombe la dunia na kuingia katika rada za usajili ni Youssef En-Nesyri (Morocco, Sevilla) Joao Felix (Portugal, Atletico Madrid), Nicolas Jackson (Senegal, Villarreal) na Enzo Fernandez (Argentina, Benfica).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live