Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoni apokewa kifalme Namungo

Nyoniiiii.jpeg Nyoni apokewa kifalme Namungo

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache tangu Erasto Nyoni atemwe na Simba kisha mabosi wa Namungo kumtambulisha kama mchezaji mpya kwa ajili ya msimu ujao, wachezaji wa timu hiyo ya mkoani Lindi wamempokea kifalme mkongwe huyo wakitaja sifa zilizombeba ikiwamo uongozi, utulivu uwanjani na nidhamu.

Nyoni ni mmoja ya wahezaji nane waliopewa 'Thank You' na Simba wiki iliyopita baada ya kuitumikia kwa misimu mitano tangu aliposajiliwa kutokea Azam FC na saa chache Namungo kupitia peji yake ilimtangaza kama usajili wa kwanza kwao.

Kutua Namungo kumemfanya kiungo mkongwe wa timu hiyo, Jacob Massawe kufunguka juu ya kujisikia fahari kwa ugeni huo wa Nyoni akisema wanaona wamepata kiongozi na mshauri wa wenzake na kwa hekima yake anaona yapo mambo yatayaongeza kwa faida kubwa kwa timu hiyo.

"Kwangu ni faraja kubwa kucheza na Nyoni timu moja, kama wachezaji tunajua heshima kubwa aliyonayo kwenye soka la Tanzania, ana nidhamu, kiongozi na mshauri unaapofanya vibaya ama vizuri hasiti kukupigia simu na kukuuliza una changamoto gani, akiweza kutatua anatatua," alisema nahodha huyo wa zamani wa Stand United, Ndanda na Gwambina United na kuongeza;

"Naamini kuna kitu kikubwa kimeongezeka Namungo, ukiachana na hilo bado ana mpira mwingi mguuni, utulivu wake uwanjani utasaidia kuwashusha wengine presha, kiukweli baada ya kumtangaza nilifurahi sana,najua umuhimu wake."

Kwa upande wa Pius Buswita, alisema Nyoni bado ni mchezaji mzuri na kwa nidhamu yake ya kazi anaona vijana wengi wanaweza wakajikuta wanasubiri kama hawatajituma na kutumia wakati wao vizuri wawapo uwanjani.

"Achana na Nyoni kucheza muda mrefu Ligi Kuu, bali kiangaliwe anachofanya uwanjani ndipo utagundua ni mchezaji wa aina gani, pia ni kiongozi anayeweza kusikilizwa na vijana wengi, kutokana na heshima aliyojijengea," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live