Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoni: Simba wanaichapa Al Ahly

Nyoni Ngaoo Nyoni: Simba wanaichapa Al Ahly

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Azizi Nyoni amesema kutokana na ubora wa timu hiyo anaipa nafasi kubwa ya kushinda mechi ya kwanza ya robo fainali ya Kombe la African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly.

Mechi hiyo imepangwa kuchezwa leo Ijumaa Oktoba 20 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 12:00 jioni ambapo inatazamiwa kuwa mgumu kutokana na ubora wa timu hizo kwa sasa.

Nyoni amesema Simba kwa sasa ina uzoefu mkubwa na mashindano ya kimataifa na wanaweza kucheza na timu yoyote ile ya hapa Afrika au hata Ulaya sababu wana wachezaji wazuri hivyo hata mchezo wa kesho anaamini itashinda.

”Nawapa nafasi kutokana na uzeofu wao Al Ahly walishakuja Tanzania miaka ya nyuma na wameshafungwa na Simba zaidi ya mara mbili sioni kama ni tishio kwa Simba”, amesema Nyoni.

Aweka wazi kwamba kikubwa wachezaji inatakiwa wasiwe na hofu wala wasidharau mchezo huo inatakiwa waichukulie kama vile fainali ya Klabu bingwa make wanaenda kucheza na timu kubwa na ngumu.

Ametumia fursa hiyo pia kuwaomba wapenzi wa Simba na mashabiki wote wa soka kwa ujumla hapa nchini kuungana kwa pamoja na kutoa sapoti ya kutosha kwa timu hiyo kesho ili iweze kupata ushindi.

“Mechi ya Power Dynamos, Bocco alirushiwa chupa za maji na mashabiki na mimi ninavyojua Simba miaka yote hawako katika maisha hayo ni wakarimu sana kikubwa niwaombe wasiwape hofu wachezaji wawashangilie”, amesema Nyoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live