Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoni, Kapombe, Tshabalala machoni mwa Pablo Franco

Nyoni (600 X 400) Erasto Nyoni atapata nafasi ya kuonekana na Kocha mpya wa Simba

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu mpya wa Simba, Pablo Franco ametua rasmi kwenye ardhi ya Tanzania tayari kwa kuanza kazi.

Kitu kizuri kwake ni kuwa amefika leo na kesho Taifa Stars itaingia uwanjani dhidi ya DR Congo katika kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Hakika hii ni fursa kwa wachezaji wa Simba watakaopata nafasi ya kucheza mchezo wa kesho kwani wakifanya vizuri itakuwa ndiyo tiketi ya kumshawishi Mwalimu awatumie kikosini akiwa na imani nzuri pamoja na kumbukumbu kuwa kama wameaminiwa na kufanya vizuri kwenye timu ya Taifa, iweje kwenye Club wakae benchi.

Fursa hii ni adimu na adhwimu kwa kina Nyoni, Kennedy, Bocco, Kibu na Mzamiru ambao bado namba zao kwenye Club hazina uhakika ukiachana na Manula, Kapombe na Zimbwe Jr ambao panga pangua wana uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza ndani ya Simba SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live