Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyiee! Kwa busta hizi, tuko pale...!

Bangala Fei Bangala na Fei Toto.

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba Sc, Yanga Sc, Azam FC na Singida Fountain Gate zimeamua. Kwa busta zilivyofungwa, tupo palee. Watu watakula nyingi kila wakikanyaga Kwa Mkapa.

Ni timu nne zitakazobeba heshima ya Tanzania Bara msimu ujao katika Mashindano ya klabu Afrika na juzi zimekamilisha kibabe vikosi vyao wakisajili jumla ya wachezaji 110.

Hatua ya kwanza ya dirisha la usajili kwa wachezaji watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho limefungwa jana rasmi Agosti Mosi kwa timu za Yanga, Singida Fountain Gate na Azam FC wakibaki Simba pekee ambao wao watanufaika na kuanza kwa ya kwanza ya ligi ya ma-bingwa ambapo wao dirisha lao litafungwa Agosti 31.

Kufungwa kwa usajili huo Yanga imeingiza wachezaji 27 huku 8 kati ya hao wakiwa wapya tayari kwa kwenda kuitetea klabu hiyo iliyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita wakiungana na wenzao wenyeji 19 ambao walisalia katika kikosi kilichopita.

Yanga imewaingiza wachezaji wapya mabeki Attohoula Yao, Gift Fred, Nickson Kibabage, viungo wakiwa Jonas Mkude, Pacome Zouzoua, Mahalatse Makudubela ‘Skudu’, Maxi Nzengeli huku mshambuliaji akiwa Hafiz Konkoni aliyechukua nafasi ya Mkongomani Fiston Mayele.

Yanga pia itakuwa chini ya kocha mpya kwenye benchi lake Muargentina Miguel Gamondi aliyekuja na wasaidizi wake Musa Nd’ew ambao wataku-wa na kazi ya kuendeleza soka kubwa lililopigwa msimu uliopita timu hiyo ilipokuwa chini ya Mtunisia Nasreddine Nabi.

Macho ya wengi watahitaji kuona Yanga itakuwa na mwendo gani watakaporejea kwenye ligi ya mabingwa ambapo msimu uliopita walishindwa kuingia makundi kisha kuangukia kombe la shirikisho ambako waliwasha moto mpaka kucheza fainali wakipoteza mchezo wa fainali ya kwanza pekee nyumbani kati ya mbili.

Kama kawaida yao Yanga hawakutaka mambo mengi wakaweka kambi yao palepale Avic Town Kigamboni walikojificha pia msimu uliopita kwenye maandalizi yao ya msimu mpya wakijifua hapo tayari kwa msimu mpya wakiwa na jeuri ya kuchukua mataji matatu ya ndani lakini pia wakicheza fainali ya shirikisho.

SIMBA

Mshindi wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita Simba naye ameshakamilisha sehemu kubwa ya kikosi chake kasoro kipa mmoja tu ambaye anatoka Amerika.Simba imeingiza wachezaji 29, lakini baadaye wakalazimika kufanya mabadiliko ya kumuondoa kipa wao mpya Jefferson Luis ambaye usajili wake umedumu kwa wiki moja pekee kabla ya juzi kumuondoa kwa madai ya kuwa na majeraha ya muda mrefu na hatoweza kuwa tayari ndani ya msimu huu.

Taarifa hiyo sasa inailazimu Simba kurudi sokoni kusaka kipa mwingine atakayeanza sambamba na Alli Salim na kinda Feruzi Tellu kufuatia kipa wao namba moja Aishi Manula naye kuwa na majeruhi akirudi uwanjani mwezi Novemba.

Ukiacha usajili huo wa kipa Simba imebakiza nafasi moja pekee ya wachezaji wa kigeni ambayo inaweza kuja kuchukuliwa na kipa huyo atakyesaji-liwa, ambapo msimu huu tayari walishakuwa wameingiza majina ya wachezaji 29 na sasa watabaki 28.

Kwenye kikosi hicho cha wachezaji 28, Wekundu hao wameshaingiza watu wapya 7 wakiwemo mabeki Che Malonde Fondoh, Hussein Kazi, viungo wakiwa Abdallah Hamis, Fabrice Ngoma, Aubin Kramo, Essomba Onana na mshambuliaji Shaban Chilunda.

Simba imepania kuwa na msimu wa mabadiliko baada ya kukosa mataji kwa misimu miwili mfululizo yaliyochukuliwa na watani wao Yanga, kuonye-sha hawataki utani msimu huu wakaamua kurudi Ulaya wakiweka kambi ya wiki tatu mjini Ankara nchini Uturuki na leo alfajiri wamerejea rasmi kuja kumalizia maandalizi yao.

Wekundu hao hawana mabadiliko makubwa kwenye benchi lao watarejea msimu mpya wakiwa chini ya kocha wao Mbrazil Robert Oliveira ‘Rob-ertinho’ ambaye ameongezewa nguvu kwenye benchi lake akiletewa wasaidizi wanne wapya wa kigeni huku aliyekuwa msaidizin msimu uliopita Juma Mgunda akipangiwa majukumu mengine.

AZAM FC

Kombe la Shirikisho Afrika kutakuwa na wawakilishi wawili tuanze na Azam FC ambao nao wamemaliza usajili wao wakiingiza kikosi chenye jumla ya wachezaji 25 ikiwa ndio timu iliyoingiza wachezaji wachache.

Azam matajiri wa pale Chamazi wao katika jeshi lao hilo la msimu ujao kuna wachezaji watano pekee ndio watazivaa jezi za kikosi hicho kwa mara ya kwanza wakisajiliwa msimu huu huku wengine 20 wakiwa wenyeji.

Katika dirisha hili Azam imewaingiza wapya Cheikh Sidibe asmbaye ni beki wa kushoto, wengine wakiwa viungo Gibril Sillah, Feisal Salum, Yannick Bangala na mshambuliaji pekee Alassane Diao.

Kama ilivyokuwa Yanga Azam nao watakuwa kwenye utawala wa kocha mpya Msenegal Youssouph Dao ambaye atakuwa na msaidizi wake Mfa-ransa Bruno Ferry, wakichukua nafasi ya Muingereza Kalli Ongala.

Kuonyesha kwamba hawataki utani Azam wakaamua kurudi tena Afrika Kaskazini safari hii wakitua nchini Tunisia wakiweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya ambapo tayari wamesharejea nchini kuja kumalizia maandalizi yao ya mwisho kabla ya kuanza mashindano.

SINGIDA

Kwa mara ya kwanza Singida watashiriki michuano ya kimataifa ikiwa ni timu changa kwenye michuano hiyo mikubwa lakini ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

SINGIDA FG

1. Benno Kakolanya(Mpya)

2. Aboubakar Khomeni

3. Benjamin Haule

MABEKI

5. Abdulmajid Mangalo

6 .Shafiq Batambuze

7. Hamad Wazir

8. Nicholas Gyan

9. Yahaya Mbegu (Mpya)

10. Biemes Carno

11. Joash Onyango (Mpya)

12. Kelvin Kijili (Mpya)

13. Nicholas Wadada (Mpya)

VIUNGO

14. Yusuf Kagoma

15. Aziz Andambwile

16. Morice Chukwu (Mpya)

17. Deuse Kaseke

18. Duke Abuya (Mpya)

19. Dickson Ambundo (Mpya)

20. Enock Atta (Mpya)

21. Bruno Gomes

WASHAMBULIAJI

22. Medie Kagere

23. Francis Kazadi

24. Thomas Ulimwengu (Mpya)

25. Bright Adjei

26. Habib Kyombo (Mpya)

AZAM FC

Makipa

2. Abdulai Iddrisu

3. Zuber Foba

4. Ally Ahamada

MABEKI

5. Edward Manyama

6. Nathaniel Chilambo

7. Daniel Amoah

8. Abdallah Kheri

9. Malickou Ndoye

10. Lusajo Mwaikenda

11. Cheikh Sidibe (Mpya)

12. Pascal Msindo

VIUNGO

13. Gibril Sillah(Mpya)

14. Sospeter Bajana

15. Feisal Salum (Mpya)

16. Yannick Bangala (Mpya(

17. James Akamiko

18. Ayoub Lyanga

19. Kipre Junior

20. Idd Seleman

WASHAMBULIAJI

22. Idris Mbombo

23. Abdul Suleiman

24. Alassane Diao (Mpya)

25. Yahya Zayd

YANGA

1. Djigui Diarra

2. Aboutwalib Mshery

3. Metacha Mnata

MABEKI

4. Attohoula Yao (Mpya)

5. Kibwana Shomari

6. Lomalisa Mutambala

7. Nickson Kibabage (Mpya)

8. Gift Fred (Mpya)

9. Bakari Mwamnyeto

10. Ibrahim Hamad

11. Dickson Job

VIUNGO

12. Pacome Zouzoua (Mpya)

13. Zawadi Mauya

14. Mudathir Yahya

15. Khalid Aucho

16. Salum Aboubakar

17. Jonas Mkude (Mpya)

18. Stephanie Aziz KI

19. Mahaltse Makudubela (Mpya)

20. Farid Mussa

21. Maxi Nzengeli (Mpya)

22. Jesus Moloko

23. Denis Nkane

Washambuliaji

24. Crispin Ngushi

25. Clement Mzize

26. Kennedy Musonda

27. Hafiz Konkoni (Mpya)

SIMBA

1. Aishi Manula

2. Ally Salim

3. Feruz Tellu

MABEKI

4. Henock Inonga

5. Mohamed Hussein

6. Shomari Kapombe

7. Che Malone Fondoh (Mpya)

8. Kennedy Juma

9. Israel Mwenda

10. David Kameta

11. Hussein Kazi (Mpya)

12. Jimson Mwanuke

VIUNGO

13. Abdallah Hamis (Mpya)

14. Fabrice Ngoma (Mpya)

15. Clatous Chama

16. Mzamiru Yassin

17. Aubin Kramo (Mpya)

18. Kibu Denis

19. Sadio Kanoute

20. Nassoro Kapama

21. Luis Miquissone (Mpya)

22. Essomba Onana (Mpya)

WASHAMBULIAJI

23. Mosses Phiri

24. Jean Baleke

25. Said Ntibazonkiza

26. Shaban Chilunda (Mpya)

27. John Bocco

28. Mohamed Mussa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: