Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyie! Kwa takwimu za Simba, Vipers anakufa mapemna tu

Simba SC Uganda 1140x640 Nyie! Kwa takwimu za Simba, Vipers anakufa mapemna tu

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi, Simba leo saa 1:00 usiku wanatarajiwa kushuka Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuvaana na Vipers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku rekodi baina yao zikiibeba mapema kwenye mchezo huo wa Kundi C.

Huo ni mchezo wa nne kwa timu hizo kundini na ni wa marudiano baina yao baada ya wiki iliyopigwa jijini Entebbe, Uganda na kushinda bao 1-0 lililowekwa kimiani na beki Henock Inonga.

Simba ipo nafasi ya tatu kundini ikiwa na pointi tatu na itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na faida kubwa ya kupata ushindi kutokana na takwimu zao za michezo mitatu iliyocheza hadi sasa tofauti na wapinzani wao ambao bado hawajafunga bao lolote.

Kwa mujibu wa mtandao wa FUTMOB, Simba iko nafasi ya pili katika kundi hilo kwa kutengeneza nafasi za hatari ambapo imetengeneza sita nyuma ya kinara Raja Casablanca iliyotengeneza 12.

Iko hivi. Licha ya Simba kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa 1-0 na Horoya ya Guinea bado ilitengeneza nafasi za hatari tatu huku mechi na Raja Casablanca iliyofungwa 3-0 ilitengeneza mbili.

Mchezo wa tatu iliyoshinda 1-0 dhidi ya Vipers, ukiwa ni wa kwanza kwenye kundi hilo ilitengeneza nafasi moja tu iliyozaa bao lililofungwa na Inonga na kuweka matumaini hai.

Kwa upande wa Vipers, takwimu zinaonyesha haijatengeneza nafasi yoyote ya hatari katika michezo yao mitatu hadi sasa iliyocheza ikiendelea kuburuza mkiani na pointi moja jambo linaloweza kuipa faida zaidi Simba katika mechi ya leo, huku Horoya iliyoko nafasi ya pili na pointi nne imetengeneza nafasi za hatari tano ikiwa ni ya tatu kundini.

Akizungumzia jambo hili, kocha wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' alisema kitendo cha kutengeneza nafasi nyingi kinaonyesha timu inacheza hivyo jukumu ni kupambana na umaliziaji tu.

"Tunahitaji kuonyesha ubora wetu zaidi ya tulivyofanya mwanzo, tuna michezo miwili mfululizo nyumbani na malengo yetu ni kupata pointi zote sita zitakazotuweka katika mazingira mazuri."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live