Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyie! Huyu Lewandowski anatisha La Liga

Robert Lewandowski El Clasico.jpeg Robert Lewandowski

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Robert Lewandowski amepondwa baada ya kuonyesha kiwango kibovu kwenye mechi ya La Liga, Barcelona ikipokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Almeria.

Lewandowski alishindwa kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi na kuipita Real Madrid kwa tofauti ya pointi 10 kwenye msimamo baada ya sare waliopata ilipocheza dhidi ya Atletico Madrid.

Unakuwa mchezo wao wa pili kufungwa msimu huu hata hivyo imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya wapinzani wao Los Blancos.

Barcelona ilijaribu kuepuka kipigo hicho na kushindwa kusawazisha bao kipindi cha kwanza, lakini kutokana na safu yao ya ushambuliaji kuwa butu wakashindwa kuingia eneo la hatari.

Mashabiki wa Barcelona walimtupia lawama Lewandowski kwasababu hakuwa makini eneo la hatari kila alipata mpira sambamba na kinda wa timu hiyo Gavi.

Takwimu zinaonyesha Lewandowski amepata asilimia 4/10, Gavi asilimia 3/10, Ferran Torres akingoza kwa asilimia 5/10, hiyo ni rekodi mbovu iliyowekwa na safu ya ushambuliaji wa Barcelona.

Kipigo hicho cha Barcelona kimeipa nguvu Madrid katika kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa La Liga msimu huu, baada ya kupoteza mwelekeo.

Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti alisisitiza licha ya timu yake kubora katika mechi zao za hivi karibuni, bado wana nafasi kwenye mbizo za ubingwa.

"Madrid bado ipo katika mbio za ubingwa, tunachotakiwa ni kupambana mpaka mwisho, baada ya hapo tutaona kitakachotokea," alisema Ancelotti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live