Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyie Azam, Biashara haoo wanakuja

Biashara Pic Data Nyie Azam, Biashara haoo wanakuja

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author USHINDI wa Biashara Utd 1-0 dhidi ya Ihefu umezidi kuwasogeza timu hiyo katika nafasi ya tatu wakitishia kuishusha Azam wanaoshikilia nafasi hiyo.

Azam wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 41 wakicheza mechi 23, wameshinda michezo 11, droo nane na kupoteza mechi nne.

Huku Biashara wao wanashika nafasi ya nne licha ya ushindi huo wakijikusanyia pointi 39 katika mechi 23 walizocheza, wakishinda 11, sare sita na kupoteza sita.

Bao la Christian Ziga linafawanya Biashara UTD kuzidi kuwa tishio msimu huu wakiwa chini ya kocha Francis Baraza ambaye ameonekana kuwa na mbinu nyingi zinazowasumbua wapinzani.

Ushindi huo pia unawafanya Ihefu waendelee kusalia katika nafasi tatu kutoka chini wakiwa na pointi 20 katika mechi 23 walizocheza mpaka sasa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz