Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyamlani 'miwili' tena TFF

Nyamlaniii (14).jpeg Nyamlani 'miwili' tena TFF

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umeridhia makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho hilo, Athuman Nyamlani kuendelea na wadhifa huo.

Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, muda wa mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo ni miaka miwili hivyo Nyamlani kwa vile alishika wadhifa huo baada ya kuteuliwa na Rais wake Wallace Karia amemaliza muda wake mwaka huu.

Kikatiba, ilipaswa Karia atangaze kumteua kwa mara ya pili, Nyamlani na kisha wajumbe wa mkutano mkuu kupitisha, jambo ambalo lilifanyika na hivyo ataendelea kuhudumu katika nafasi hiyo ambayo pia inamfanya awe Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ya TFF.

"Na kwa vile naye ni miongoni mwa wajumbe niliowateua, nilikuwa nawaomba wajumbe mridhie Athuman Nyamlani aendelee kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa TFF," amesema Karia.

Baada ya Karia kutangaza hivyo, wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wamepitisha uteuzi huo na hivyo Nyamlani ataendelea kuhudumu kwa miaka miwili ijayo.

Mbali na Nyamlani, wajumbe wa mkutano huo, wamepitisha uteuzi wa Ahmed Mgoyi, Said Soud na Hawa Mniga kuwa wajumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya TFF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live