Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyakati zimekwenda wapi kwa Harry Maguire?

Harry Maguire After Man Utd Concede A Goal Harry Maguire

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tarehe 11 August 2019, katika uwanja wa Old Trafford Harry Maguire alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi cha Manchester United, dhidi ya Chelsea.

United walitoa kiasi cha £80m kwa Leicester City Ili kumpata Maguire ambaye alikuwa ni moja kati ya wachezaji bora wa Leicester City misimu miwili nyuma.

Clearances 7, Blocks 2, Interceptions 4 - hizi zilikuwa ni takwimu za Maguire kwenye debut yake dhidi ya Chelsea ndani ya dakika 90 alizocheza.

Baada ya mchezo Maguire alisema yeye na wenzake wanaocheza eneo la ulinzi wataifanya ngome ya Man United kuwa ngumu kuingilika, Man United itakuwa ngumu kufungika.

Siku na miezi kadhaa baadae alitangazwa kama captain baada ya kuwa kwenye nyakati nzuri pale United.

Huyu Maguire yupo wapi? Where is old Maguire? Leo hii picha ya Maguire inatumika kama vichekesho kwenye social media.

Tusubiri, majibu tutayapata. Mpira una mambo mengi sana. Phil Jones alishawahi kuzungumza kuhusu maisha yake ya mpira yalivyokuwa magumu kwa miaka mingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live