Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyakati za furaha kurejea Simba SC

Simbasctanzania 248553240 3739045686198117 3280563547585519395 N 1 Simba wapata ahueni kurejea kwa nyota wao

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kurejea kwa nyota wawili wa klabu hiyo, Pape Ousmane Sakho na Chris Mugalu ambao tayari wameanza mazoezi baada ya kukosekana kwenye michezo minne iliyopita kutokana na majeraha.

Mugalu na Sakho walipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Oktoba Mosi mwaka huu, ambapo kutokana na majeraha hayo mpaka sasa wamekosa michezo minne ya Simba katika mashindano yote.

Simba imeanza kwa kusuasua msimu huu ambao mpaka sasa wanakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi nane tu katika michezo minne waliyocheza mpaka sasa. Leo Simba wanatarajiwa kuikaribisha Namungo kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry amesema: “Baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha, tunatarajia wachezaji Sakho na Chris Mugalu watarejea kikosini baada ya kupona majeraha yao.

“Wachezaji hao wote wawili tayari wameanza programu za mazoezi, na kuendana na mahitaji ya benchi la ufundi tuna matumaini makubwa watakuja kuongeza nguvu katika michezo ijayo.”

Chanzo: globalpublishers.co.tz