Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nusu fainali ya EURO 2024 itakuwa patashika

Euro 2024: Ureno Na Ufaransa Zafuzu Kwa Robo Fainali Ya Euro Nusu fainali ya EURO 2024 itakuwa patashika

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uholanzi imejikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya kandanda kwa maitaifa ya Ulaya EURO 2024.

Ushindi huo katika mchezo uliopigwa mjini Berlin umefufua matumaini ya timu hiyo kulikaribia kombe la EURO ambalo walilinyakua kwa mara ya mwisho mwaka 1988. 

Uholanzi itakuwa na kibarua kigumu pale itakapokutana na England kwenye mchezo wa nusu fainali uliopangwa siku ya Jumatano ya wiki ijayo. 

England nayo ilisonga mbele hapo jana kupitia mikwaju ya penalti ya 5-3 katika mchezo uliowakutanisha na timu ya taifa ya Uswisi. Timu nyingine mbili zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni Ufaransa na Uhispania ambazo zina miadi mnamo siku ya Jumanne. 

Ufaransa ilipata ushindi dhidi ya Ureno kupitia penalti na Uhispania iliwafungasha virago wenyeji Ujerumani kwa mabao 2-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live