Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nusu fainali CAFCL ni wakubwa tu

Al Ahly Vs Simba 2 0.jpeg Nusu fainali CAFCL ni wakubwa tu

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba na Yanga tayari zimeaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukosa matokeo ya kuzivusha kutoka robo fainali kwenda nusu fainali hatua ambayo zimeingia timu nne ambao ni vigogo wa Afrika waliosheheni uzoefu na rekodi kwenye michuano ya CAF.

Simba imegota katika nusu fainali hiyo kwa mara ya nne sasa ndani ya miaka sita baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-0, ikifungwa 1-0 nyumbani na kuchapwa 2-0 ugenini huku msimu wa 2020-2021 ikiishia pia robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo kiufupi katika miaka nane imeishia robo fainali za CAF mara sita.

Kwa upande wa Yanga licha ya kufurukuta lakini imeshindwa kupenya robo faianali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutolewa na Mamelodi Sundowns kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya matokeo ya jumla kuwa 0-0 katika mechi mbili nyumbani na ugenini.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Yanga kufika hatua hiyo kwa miaka ya hivi karibuni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini msimu uliopita ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho na bingwa kukosa ubingwa kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2, ikifungwa Kwa Mkapa 2-1 na kushinda ugenini 1-0.

KIKUBWA ZAIDI

Ukiachana na malalamiko yanayoendelea baina ya timu hizo mbili, nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu zimeingia timu nne vigogo tu.

Ni Bingwa mtetezi, Al Ahly ambaye ametwaa taji hilo mara nyingi zaidi akilibeba mara 11. Kiufupi Al Ahly ndio wafalme wa soka la Afrika kutokana na rekodi mbalimbali walizonazo ikiwemo kutwa kombe la Shirikisho mara moja mwaka 2014 na kuwa timu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji la Caf Super Cup ikinyanyua kombe hilo mara nane. Ahly imetinga robo fainali kwa kuitoa Simba.

Timu nyingineni ni Esperance Sportive de Tunis ya Tunisia. Hawa ni wakali kutoka Tunisia ambao tayari wamefanya makubwa mengi kwenye michuano ya CAF wakibeba taji la Ligi ya Mabingwa mara nne mwaka 1994, 2011, 2018 na 2019. Aidha Esperance wametwaa Caf Super Cup mara moja mwaka 1995. Esperance imefika hapa kwa kuitoa Asec Mimosas kwa matuta 4-2 baada ya matokeo ya jumla kuwa 0-0.

Timu nyingine nyingine ni Mamelodi iliyowatoa Yanga. Hawa ni wakali wengine kutoka Afrika ambao wamefanya makubwa kwenye michuano ya CAF wakitwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara moja mwaka 2016, Caf Super Cup mara moja mwaka 2017 na African Football League mara moja msimu uliopita ikiwa ni msimu wa kwanza wa mashindano hayo.

Msimu uliopita iliishia nusu fainali na kutolewa na Wydad Casablanca kwa faida ya bao la ugenini matokeo ya jumla yakiwa 2-2. Mamelodi wamefika hapo kwa kuitoa Yanga.

Wakali wengine waliotinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ni Tout Puissant Mazembe, (TP Mazembe), kutoka DR Congo. Hii ni miamba ya Afrika na imefanya makubwa kwenye michuano ya CAF ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu, mwaka 2009, 2010 na 2015 pia imebwba kombe la Shirikisho mara mbili mwaka 2016 na 2017 na kutwa taji la CAF Super Cup mara tatu mwaka 2010, 2011 na 2016.

Wakongomani hawa wameamka msimu huu baada ya kusinzia kwa misimu mitatu nyuma na wametinga hatua hiyo kwa kuwatoa Petro de Luanda ya Angola kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 ikitoa sare tasa nyumbani na kushinda 2-1 ugenini katika mechi ya mwisho. Timu yako inarekodi gani mbele ya vigogo hawa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live