Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nusu Fainali ya CHAN kitawaka leo

WhatsApp Image 2023 01 31 At 13.jpeg Nusu Fainali ya CHAN kitawaka leo

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michezo ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN) inafanyika leo huko Algeria.

Katika nusu fainali ya kwanza wenyeji Algeria itakipiga dhidi Niger kwenye uwanja wa Miloud Hadefi uliopo mjini wa Oran.

Kutinga hatua hiyo Algeria imeitoa Ivory Coast wakati Niger imeiondosha Ghana.

Wawakilishi pekee kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati, Madagascar itakuwa dimbani katika nusu fainali ya pili kuivaa Senegal kwenye uwanja wa Nelson Mandela uliopo jiji la Algiers.

Madagascar imefuzu hatua hiyo baada ya kuitoa Msumbiji wakati Senegal imeitupa nje Mauritania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live