Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nuno: Mpira wa Miguu Hauna Huruma

Nuno Espirito Santo 5567015 696x392 Kocha alietimuliwa kazi Tottenham, Nuno Espirito Santo

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nuno Espirito Santo ameelezea kwamba “Mpira wa miguu ni mchezo usiyo na huruma” lakini anaendelea mbele kuangalia changamoto mpya baada ya kutimuliwa na Tottenham wiki iliyopita.

Kocha huyo wa raia wa Ureno aliweza kuisamimia Spurs kwa mechi 10 pekee za Premier League kabla ya kufungishwa vilago.

Nuno ambaye alisaini dili ya miaka miwili na klabu hiyo ya kasikazini mwa London lakini iliweza kudumu kwa miezi minne na kufika mwisho hivi karibuni na nafasi yake kuchuliwa na Antonio Conte.

Kocha huyo wa zamani wa Wolves wiki chache zilizopita aliweka post kwenye akaunti yake ya Instagram akisisitiza anajifunza kutokana na uzoefu mgumu anaopitia.

“Huu mchezo wa mpira wa miguu hauna huruma sana, wiki nyingi zilizopita nilikuwa nikipokea tuzo ya kocha bora wa mwezi na muda mchache badaye nimeondolewa Spurs.

“Haya ni maisha nasonga mbele kuangalia changamoto nyingine. Ningependa kuwashukuru mashabiki wa Spurs nilipojiunga na Spurs malengo yangu yalikuwa ni kushinda mataji lakini mpnago haukwenda vyema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live