Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nunez apiga goli 2 Liverpool ilichukua pointi 3

BF6143E7 D014 4EE3 9CE4 7B649376A872.jpeg Darwin Nunez alifunga magoli 2

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Liverpool jana wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Roberto Firmino dakika ya sita na mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Darwin Nunez dakika ya 21 na 42, wakati la Southampton lilifungwa na mshambulaji wa kimataifa wa Scotland mzaliwa wa England, Che Zach Adams dakika ya tisa.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya sita, wakati Southampton inabaki na pointi zake 12 za mechi 15 nafasi ya 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live