Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nunez aigharimu pesa ndefu Liverpool

Darwin Nunez3 1200x630 Darwin Nunez

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool inajidaa kuilipa Benfica Pauni 8.5 milioni baada ya Darwin Nunez kufikisha mechi 60 alipocheza dhidi ya Manchester City wikiendi iliyopita.

Gazeti la Mirror limeripoti baada ya kujumuishwa kikosini wikiendi iliyopita Liverpool itatoa pesa kama sehemu ya makubaliano katika kipengele cha mkataba wake.

Liverpool ilimsajili Nunez rekodi ya usajili wa Pauni 85 milioni, aidha ilitoa Pauni 64 milioni kwanza na Pauni 21 milioni itatolewa.

Liverpool ililipa Benfica Pauni 4.3 milioni baada ya mshambuliaji huyo kucheza mechi 10 na sasa ipo tayari kulipa Pauni 8.5 milioni baada ya kufikisha idadi hiyo ya mechi.

Umekuwa mwanzo mzuri kwa Nunez msimu huu, akiwa tayari amefunga mabao 12 na asisti saba katika mechi 16 alizoanza.

Hata hivyo, baadhi ya magwiji wa soka bado hawana imani kama Nunez atakuwa mfungaji bora wa muda wote Liverpool, huku mkongwe wa Liverpool, Robbie Fowler miongoni wanaohofia kiwango chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live