Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nugaz, Nado wazua gumzo tuzo za TFF

Pjimage (41) Waliozua gumzo katika vipengele vya tuzo za TFF

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliekuwa Afisa muhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz, amezua gumzo kwa wadau, wapenzi na mashabiki wa soka baada ya kutoonekana jina lake katika tuzo zitakazotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, kipengele cha Muhamasishaji bora.

Walio wengi wameona kuna makosa makubwa katika kipengele hicho kwa kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Bodi ya Ligi wiki chache zilizopita , Yanga ndio timu iliyoongoza kwa Mashabiki wake kuhudhuria viwanjani msimu wa 2020/2021 na muhamasishaji wao alikuwa ni Antonio Nugaz.

Kipengele hicho kimewahusisha Aliekuwa afisa Habari wa Simba msimu Uliopita Haji Manara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire na Nicholas Reynolds maarufu kama "Bongo zozo"

wengi wamekosoa uteuzi huo na kudai tuzo hiyo ilipaswa kwenda moja kwa moja kwa Nugaz na haikuwa sahihi kuiweka kama tuzo ya kugombaniwa.

Vile vile, gumzo jingine lilikuja kwa kiungo wa Azam, Iddy Nado ambae amekuwa na msimu mzuri kwa kuhusika katika magoli takribani 18 ndani ya kikosi cha Azam FC lakini jina lake halijatokea katika kipengele chochote kile katika tuzo hizo za TFF.

Nado anazidiwa na aliekuwa kiungo wa Simba Clatous Chama kwa kuhusika katika magoli mengi lakini cha ajabu hayumo katika vipengele vya tuzo hizo, hali ya kuwa wachezaji waliocheza chini ya ubora wake wameteuliwa kuwania baadhi ya tuzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live