Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza sasa ampa jeuri Kaze

E4459b17a98202710cd557045c0d2d27 Ntibazonkiza sasa ampa jeuri Kaze

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KIWANGO kilichooneshwa na mshambuliaji mpya wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza kinampa jeuri Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Cedric Kaze baada ya kukunwa na kiwango chake na kumsifia kuwa anajua kulisakata kabumbu.

Ntibazonkiza alicheza mchezo wa kwanza juzi dhidi ya Singida United akiwa na klabu yake hiyo mpya aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la usajili na kutupia mabao mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Liti Singida.

Bao jingine katika mchezo huo lilifungwa na Deus Kaseke ambaye naye amekuwa katika kiwango bora akitupia katika mechi mfululizo za Ligi Kuu.

Baada ya mchezo huo wa juzi Kaze alisema Ntibazonkiza ameonesha kile ambacho anakijua kutoka kwake.

“Ni mchezaji mzuri ameonesha kile tulichotarajia, anajua kuchezesha timu na kuongoza wenzake uwanjani,” alisema Kocha huyo raia wa Burundi.

Kwa upande wake, Ntibazonkiza alisema anashukuru kwa kupata nafasi ya kucheza katika mchezo huo wa kirafiki na kumaliza bila majeruhi na kwamba alichokionesha ni cha mtoto kwani kazi nzuri inakuja mbele.

Alisema amekuja kutumia uzoefu wake kuisaidia Yanga ili kuona kama na wanachezaji wenzake watafikia malengo yaliyokusudiwa ya kutwaa ubingwa.

Yanga iliyotoka Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui na kushinda mabao 5-0, ilipita Singida na kujipima na Singida United ikitumia zaidi wachezaji wake ambao hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa mkoani Arusha Jumamosi.

Kaze aliutumia mchezo huo wa kirafiki kuwapa nafasi wachezaji wake wanaokosa namba kikosi chake ili kuwaimarisha.

“Tumeona tuwape nafasi wachezaji ambao hawapati namba kwenye kikosi cha kwanza ili kuwajengea uzoefu na kujiamini,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz