Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza kuivaa Prisons, Simba ikitambulisha mashine

Saido Simba Ths Saido Ntibazonkiza

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kiungo mpya, Saido Ntibazonkiza, anatarajiwa kuanza kuitumikia timu yake ya Simba kesho katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons, klabu hiyo huenda ikatangaza mchezaji mpya iliyemsajili kwenye dirisha dogo ambalo limefunguliwa.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema wanatarajia kukamilisha taratibu zote muhimu kesho na mambo yakienda vyema, Ntibazonkiza atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani kuwakabili Maafande wa Prisons.

Ahmed alisema mchezaji huyo yuko tayari kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba na wanaamini ujio wake utawasaidia.

"Siku hiyo uwanjani itakuwa ni kama sherehe kwa wanachama na mashabiki wa Simba, tunakwenda kuuaga mwaka 2022, kwenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwenda kupongezana Wanasimba, kukosoana na kuulizana kuanzia kwenye timu yetu na hata maisha ya kawaida kama wanadamu, " alisema Ahmed.

Aliongeza klabu hiyo inaendelea na mchakato wake wa kusajili na huenda pia kesho wakatambulisha mchezaji mpya kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Mwenyekiti wa Bodi (Salim Abdallah) ameniambia analifanyia kazi hilo, likiwezekana atanijulisha kwa hiyo Ijumaa itakuwa ni mechi fulani hivi ya Wanasimba na baada ya hapo wakazi wa Dar na Tanzania Bara hawataiona tena timu kwa sababu itaelekea Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi," alisema kiongozi huyo.

Aliongeza wanachama na mashabiki wa Simba wasikaririshwe majina ya wachezaji wanaodaiwa wanasajiliwa na badala yake wasubiri taarifa rasmi ya klabu.

"Tunaendelea na usajili wa wachezaji wapya, wanachama na mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi, wanatakiwa kukaa wakisubiri  mchezaji yoyote atakayekuja kuisaidia timu na siyo jina la mtu au lazima aje mchezaji fulani," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live