Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza apewa Prisons

Saido Simba Ths Ntibazonkiza apewa Prisons

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa Saidi Ntibazonkiza amepewa shavu la kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ambacho muda mchache ujao kitacheza dhidi ya Mafaande wa Tanzania Prisons kwa Mkapa.

Nyota huyo ambaye amejiunga na Simba akitokea Geita Gold kwa mkataba wa miaka miwili wakati wa dirisha hili la usajili hii itakuwa mara yake ya kwanza kuwatumikia wekundu hao wa Msimbazi.

Licha ya ugeni wake, kocha wa Simba, Juma Mgunda ameamua kumtishwa mabomu mshambuliaji huyo ili aongoze safu yake sambamba na John Bocco.

Ntibazonkiza ambaye aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kwenda Geita anatazamwa kama mchezaji ambaye anaweza kuongeza makali kwenye safu hiyo ya ushambuliaji kutokana na kukosekana kwa Moses Phiri ambaye ni majeruhi.

Kikosi kamili cha Simba kinaundwa na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Joash Onyango, Hennock Inonga, Sadio Kanoute, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, Bocco, Ntibazonkiza na Pape Sakho.

Chanzo: Mwanaspoti