Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza aanzia benchi

Saido Pic Data Ntibazonkiza aanzia benchi

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

STRAIKA mpya wa Yanga, Saido Ntibazonkiza ameanzia benchi katika mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Sheikh Abeid.

Hii inakuwa kama ambavyo ilivyokuwa katika mazoezi ya jana jioni baada ya Kaze kumuanzisha Kaseke akicheza sambamba na Yacouba pamoja na Sarpong, kisha baadae alimtoa Kaseke na kuingia Saido.

Katika kikosi cha leo kocha Kaze amewaanzisha Deus Kaseke, Yacouba Sogne na Michael Sarpong katika eneo la ushambuliaji.

Kikosi hiki hakina mabadiliko makubwa na kile kilichocheza dhidi ya Mwadui, bali tu katika benchi ameondoka Paul Godfrey na kuingia Saido Ntibazonkiza.

Kikosi kilichoanza ni Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto.

Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Tuisila Kisinda, Deus Kaseke, Michael Sarpong na Yacouba Sogne.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz