Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza aanza dhidi ya Singida

Ntiba Pic 1 Data Ntibazonkiza aanza dhidi ya Singida

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

STRAIKA mpya wa Yanga, Said 'Saido' Ntibazonkiza ameanza katika kikosi cha kwanza kitakachocheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Singida United, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Liti leo saa 10:00 jioni.

Yanga inacheza mchezo huo wa kirafiki na klabu hiyo ya Ligi Daraja la kwanza, ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Jumamosi, Disemba 19 uwanja wa Sheikh Abeid, Arusha.

Saido hii ni mara ya kwanza kuvaa jezi ya Yanga katika mechi  baada ya awali kusajiliwa kisha  kurejea nyumbani kwao Burundi.

Mchezaji huyo katika kikosi cha Yanga ameamuachia jezi namba 10, Yacouba Sogne kisha yeye amechukua jezi namba 60 ambayo ilikuwa haivaliwi na yeyote.

Katika kikosi hiko pia kocha Cedric Kaze amemuanzisha mshambuliaji Waziri Junior ambaye alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika mechi za Ligi Kuu.

Waziri atacheza sambamba na Saido katika eneo la ushambuliaji katika mchezo huu wa kirafiki ambao ni maalum kwa wachezaji kupata utimamu wa mwili.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz