Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza, Nahimana waitwa Burundi

NTIBAZONKIZA V4 Ntibazonkiza, Nahimana waitwa Burundi

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NYOTA Saido Ntibazonkiza anayecheza katika kikosi cha Yanga amejumuishwa kwenye timu ya Taifa Burundi kwa ajili ya mechi za kirafiki.

Burundi inajiandaa kucheza  mechi mbili za kirafiki dhidi ya Comoro na Mynamar itakayopigwa Novemba 10 na 13.

Ntibazonkiza licha ya kutojumuishwa mara kwa mara katika klabu ya Yanga amepata nafasi hiyo kwenye kikosi kilichotangazwa.

Nyota wengine wanaocheza Ligi ya Tanzania na wameitwa katika timu hiyo ni Jonathan Nahimanana Brigimana Blaise wote wa Namungo na Steven Nzigamasabo wa Mtibwa Sugar.

Kikosi kilichoitwa makipa ni Justin Ndikumana, Arthur Arakaza na Jonathan Nahimana.

Mabeki ni Weymans Marco, Oslev Nzeyimana, Eric Ndizeye na Omar Moussa.

Viungo Ndayishimiye Youssuf, Nshimirimana Jospin, Christophe Nduwarugira, Saido Ntibazonkiza, Steve Nzigamasabo, Brigimana Gael, Iruntingabo Tresor na Irakoze Piclaire.

Washambuliaji ni Saido Berahino, Fiston Abdoul, Amissi Mohamed, Kanakimana  Bienvenue, Amiss Cedric, Blaise Bigirimana na Bimenyimane Caleb.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz