Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibazonkiza Ampagawisha Nabi Yanga

Nabisaido Pic Data Ntibazonkiza Ampagawisha Nabi Yanga

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BIG bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Nasreddine Nabi ameonekana kukoshwa vilivyo na kiwango cha staa wake, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ huku akiwaambia viongozi wa timu hiyo wampe mkataba mpya.

Saido amekuwa na kiwango cha juu ndani ya kikosi hicho msimu huu akiwa amefunga mabao manne na asisti moja katika ligi. Nyota huyo pia anakaribia kumaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimesema kwamba uwezo wa nyota huyo umefanya kocha huyo awaambie mabosi wake wampe mkataba.

“Tangu Saido aanze kucheza kwenye kikosi amemshawishi sana kocha Nabi kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha ambapo ameutaka uongozi kumuongezea mkataba.

“Ukiangalia Saido amehusika kwa asilimia kubwa katika mabao ya Yanga, kitu ambacho Nabi ameonekana kuvutiwa nacho na kwa sasa huwezi kumwambia kitu chochote kuhusu Saido yaani anamkubali sana.”

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa: “Saido amekuwa na kiwango kizuri lakini kwa sasa tunafikiria kumuongezea mkataba.

“Ukiangalia katika michezo ya hivi karibuni amekuwa na kiwango kizuri sana hata wewe ungeacha kumpa mkataba sasa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live